Event date: 8/1/2016 - 8/8/2016 Export event
Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) yalifanyika Mkoani Lindi katika Viwanja vya Ngongo kuanzia tarehe 01/08/2016 hadi 08/08/2016. Ujumbe wa maonesho hayo ulikuwa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Nguzo ya Maendeleo, Kijana Shiriki Kikamilifu “Hapa Kazi tu”.
Katika maonesho hayo Wakala ulishiriki pamoja na wadau ambao ni:
Katika maonesho hayo, Wakala ulipata fursa ya kuelezea mpango wake wa kusambaza umeme vijijini na kuonesha picha za wanufaika wa miradi ya REA katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na mikoa mingine (video documentary) na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu miradi ya kusambaza nishati bora vijijini.
Wananchi wengi waliofika katika banda la Wakala walitoa pongezi na shukrani kwa kupelekewa huduma ya umeme kupitia miradi ya kusambaza umeme vijijini. Hata hivyo, walijitokeza baadhi ya wananchi waliolalamikia baadhi ya vijiji vyao kutofikiwa na miundo mbinu ya umeme na kuomba maelezo ya mpango endelevu wa kusambaza umeme vijiji vyote Tanzania Bara.
Jaina D. MsuyaAfisa Habari na Elimu kwa UmmaWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, Tanzania
Barua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007