News Centre

MEM NEWS BULLETTIN: REA YATAKA USHIRIKIANO TAASISI ZA KIFEDHA, SEKTA BINAFSI

Friday, August 7, 2015|Number of views (3945)|Categories: News

Documents to download

MEM NEWS BULLETTIN: REA YATAKA USHIRIKIANO TAASISI ZA KIFEDHA, SEKTA BINAFSI

Taasisi za Kifedha, Sekta Binafsi na Washirika wa Maendeleo nchini, wameshauriwa kutumia fursa zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kushirikiana na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji vingi zaidi na umeme, ikiwemo kuwezesha mapinduzi ya maendeleo kupitia nishati hiyo.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na REA, kikijumuisha Taasisi za Kifedha, Sekta Binafsi, Washirika wa Maendeleo, Washirika katika tasnia ya nishati, na wawakilishi kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, kwa lengo la kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja ili kuongeza nguvu ya kuhakikisha Tanzania hususan vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme ili kuchochea shughuli za kiuchumi vijijini.

Akifungua kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, alisema, miradi ya kuviunganisha vijiji na nishati ya umeme ni eneo linalohitaji kuendelezwa kwa ushirikiano na wadau hao ili kuongeza kasi ya uunganishaji umeme.

Alisema kuwa, tangu Wakala huo kuanzishwa mwaka 2007 kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme imeongezeka, na kuongeza kuwa, jitihada kubwa imekwishafanywa na Serikali na endapo wadau hao wataunganisha nguvu, azma ya serikali kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 taifa zima liwe limeunganishwa na nishati hiyo litafikiwa haraka kwa kuwa REA itakuwa na vyanzo vingi vya fedha.

Mwihava aliongeza kuwa, serikali imefanikiwa kuimarisha miundombinu ya uzalishaji umeme jambo ambalo limewezesha kiwango cha uzalishaji kuongezaka kutoka megawati 891 mwaka 2005 hadi 1,226.3, Machi 2015.

“Ikiwa vijiji vyetu vitaunganishwa na nishati hiyo, hali hiyo itachochea shughuli za kiuchumi kufanyika ikiwemo kuanzishwa kwa viwanda vidogo katika maeneo ya vijijini, na kuongeza huduma za kisasa za kiuchumi zinazotumia nishati hiyo. Umeme ni maendeleo na ili tuendelee tunahitaji umeme,” alisema Mwihava.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Edmund Mkwawa, alieleza kuwa, endapo wadau hao watashirikiana na REA, mradi huo utaleta matokeo makubwa zaidi ya yaliyopatikana sasa na hivyo kuweza kuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo. Aliongeza kuwa, zipo fursa nyingi ambazo taasisi hizo zinaweza kuzitumia kupitia miradi mbalimbali ambayo itawezesha kupata faida na hivyo, kikao hicho kitawawezesha wadau hao kutambua fursa hizo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa REA, Dkt. Lutengano Mwakahesya alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote ambao wamewezesha Wakala huo kuunganisha miji, vijiji na nishati hiyo kufikia asilimia 40 na kueleza kuwa, Wakala huo utaendelea kutafuta wafadhili ili kuweza kufanikisha malengo yake ya kuhakikisha kwamba taifa linaunganishwa na umeme.

Aliongeza kuwa, serikali peke yake haiwezi kufanya kazi hiyo na kueleza kuwa, uhakika wa uwepo wa umeme utawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi anayeshughulikia nishati kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Stella Mandago, alizitaka taasisi hizo kufanya kazi na Wakala huo kwani zipo fursa nyingi na hivyo itawezesha taasisi hizo kupanua wigo wa shughuli zao kiuchumi kupitia nishati ya umeme.

Na Asteria Muhozya
MEM News Bullettin Toleo No. 78


Documents to download

«April 2017»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
101112
93

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Pwani uliofanyika tarehe 13/03/2017 katika kijiji cha Msufini Wilaya ya Kibaha.
Read more
13
94

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA DODOMA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Dodoma uliofanyika tarehe 16/03/2017 katika kijiji cha Kigwe Wilaya ya Bahi.
Read more
14
95

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MARA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Mara uliofanyika tarehe 18/03/2017 katika kijiji cha Mariwanda Wilaya ya Bunda.
Read more
1516
97

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA IRINGA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Iringa uliofanyika tarehe 21/03/2017 katika kijiji cha Image Wilaya ya Kilolo.
Read more
17
98

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA SINGIDA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Singida uliofanyika tarehe 24/03/2017 katika kijiji cha Mkwese Wilaya ya Manyoni.
Read more
1819

Energy Access Situation Report, 2016 Tanzania Mainland

This Survey Report is the second product of the Rural Energy Agency (REA) under the Ministry of Energy and Minerals. The first one was conducted in 2011 aimed at providing baseline data on the access and use of energy in Tanzania Mainland.
Read more
20
92

UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

Mhe. Prof. Sospeter M. Muhongo (Mb.), Waziri wa Nishati na Madini, amemteua Mwenyekiti na Wajumbe Wapya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kutokana na Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu Nambari 5(1) (b) Nambari 8(3) cha Sheria ya Nishati Vijijini ya Mwaka 2005.
Read more
212223
24252627282930
1234567