News Centre

LINDI NA MTWARA WAPATA MIJI WASHIRIKA KUTOKA NORWAY

Wednesday, October 2, 2013|Number of views (6562)|Categories: News
LINDI NA MTWARA WAPATA MIJI WASHIRIKA KUTOKA NORWAY

Waziri wa Nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wa miji miwili ya Hammerfest na Sandnessjoen iliyoko nchini Norway wamekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya miji hiyo na ile ya Lindi na Mtwara.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa miji hiyo na ujumbe wa wizara ya nishati na madini nchini Norway ambapo wamekubaliana kukutana mwezi ujao kuweka mikakati ya ushirikiano huo.

Katika makubaliano hayo viongozi kutoka pande zote wamekubaliana kuwa mji wa Harmmerfest utashirikiana na Lindi na ule wa Sandnessjoen utashirikiana na Mtwara, ushirikiano ambao unalenga kuzitumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza mara baada ya kufikia makubaliano hayo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo amesema ili kuhakikisha mikoa ya kusini inanufaika na rasilimali zake, Serikali imeamua kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kutimiza azma hiyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa wavuvi katika mji wa Sandnessjoen amesema uhusiano mzuri kati ya serikali na makampuni ya mafuta umechangia kubadilisha historia ya watu wa maeneo hayo ikiwemo kuwawezesha kukua kichumi na kuwasaidia kupata huduma mbalimbali za kijamii.

Akizungumzia umuhimu wa makampuni ya mafuta katita mji wa Sandnessjoen Meya wa mji huo Bard Anders Lango amesema, kwa kiasi kikubwa mapato ya mji huo yanatokana na mafuta.

Aidha Lango ameongeza kuwa asilimia ishirini na mbili ya mapato yanayotokana na Mafuta inatumika kutoa huduma muhimu za kijamii katika sekta za afya na elimu.

Naye Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Mafuta la BP Olav Fjellsa amesema moja ya mbinu ambazo zimeliwezesha shirika hilo kujenga mahusiano mema na jamii ni kuhakikisha yanatoa misaada katika maeneo husika, kuwekeana mikataba mizuri pamoja na kujihusisha na ununuzi wa bidhaa za wazawa.

Kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya miji hiyo na mikoa ya kusini kutasaidia kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na hiyvo kuwezesha wananchi kuwa sehemu ya mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi ya umma katika maeneo yao.

Kabla ya ugunduzi wa Gesi na Mafuta miji hiyo miwili ilikuwa ikijishughulisha na uvuvi, kabla ya Serikali ya Norway kuamua kuanzisha shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta baada ya kufikia makubaliano na wananchi wa maeneo hayo.


Imeandaliwa na:

Nuru I. Mwasampeta
Afisa Habari
Wizara ya Nishati na Madini
754/33, Samora Avenue
S. L. P. 2000
Dar es Salaam, Tanzania
info@mem.go.tz
www.mem.go.tz


«February 2017»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
6789

UTEKELEZAJI WA MRADI KABAMBE WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (TURNKEY III) WAANZA

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeanza utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Awamu ya Tatu utakaojumuisha vijiji 7,873 katika wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara. Kati ya vijiji hivyo, vijiji 7,697 vitapelekewa umeme wa gridi na vijiji 176 umeme wa nje ya gridi (off-grid).
Read more
101112
13141516171819
2021

TANGAZO LA MAFUNZO KWA AJILI YA MAFUNDI NA WAENDELEZAJI WA VYANZO VYA UMEME UNAOZALISHWA KUTOKANA NA NISHATI JADIDIFU

Wakala wa Nishati Vijiji (REA), kwa kipindi cha robo ya mwisho (Aprili – Juni) ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 umepanga kutoa mafunzo kwa mafundi na waendelezaji wa vyanzo vya umeme unaozalishwa kutokana na raslimali za nishati jadidifu katika kila mkoa Tanzania Bara.
Read more
2223242526
272812345
6789101112