News Centre

NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI

Saturday, April 13, 2013|Number of views (6773)|Categories: News
NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI

Serikali ya Tanzania imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada wa Krona milioni 700, sawa na shilingi bilioni 200 za Tanzania, kutoka Serikali ya Norway, kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisaini mkataba wenye makubaliano hayo, Aprili 9, 2013 Mjini Oslo Norway akiiwakilisha Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Norway iliwakilishwa na Waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Heikki Holmas.

Zoezi la kusaini mkataba huo lilifanyika mwishoni mwa Mkutano ambao Waziri Muhongo alishiriki uliobeba dhima isemayo ‘Nishati na Maendeleo Kuanzia 2015’. Malengo mahsusi ya mkutano yalikuwa ni kufanya majumuisho ya majadiliano mbalimbali kuhusu nishati ambayo yamekuwa yakifanyika ulimwenguni kote na katika mitandao, na pia kutoa mapendekezo kuhusu nafasi ya nishati katika maendeleo kuanzia mwaka 2015.

Akizungumzia msaada huo, Prof. Muhongo alisema “sasa tunao uhakika wa kumaliza miradi ya umeme kwenye Wilaya mpya 13, zoezi litakalogharimu takribani shilingi bilioni 70 za kitanzania, na pia kukamilisha miradi mingine ya umeme vijijini”.

Kwa upande wake, Waziri Holmas alisema “kuwapatia watu waishio vijijini huduma ya umeme ni sawa na kuwapatia Watanzania wengi uwezekano wa kuondokana na matumizi ya nishati zenye uharibifu kama mafuta ya taa na dizeli.” Alifafanua kuwa msaada huo unalenga kuleta usawa kwa vitendo, ambao utainua hali ya maisha haraka na kuleta njia mbadala za kujipatia kipato kwa wananchi wa vijijini.

Alisema, zaidi ya asilimia 90 ya msaada uliotolewa itatumika kuweka umeme kwa kuongeza miundombinu ya usambazaji wa umeme, ambapo kwa mujibu wake ndiyo namna nzuri zaidi ya kuyafikia maeneo ya vijijini kwa huduma husika, kulingana na uzoefu.

Profesa Muhongo alisema Tanzania imedhamiria kuongeza huduma ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa Watanzania kutoka asilimia 18.4 hadi 30 kwa ngazi ya taifa, na kutoka asilimia 6.5 hadi 15 kwa maeneo ya vijijini.

Baada ya Mkutano na makubaliano hayo, Waziri Muhongo ameendelea na safari yake katika Mji wa Brussels, Ujerumani akiendelea na zoezi la kutafuta fedha za miradi mbalimbali ya umeme.

Imeandaliwa na:

Fadhili P. Kilewo
Mkuu wa Idara ya Habari
Wizara ya Nishati na Madini
754/33, Samora Avenue
S. L. P. 2000
Dar es Salaam, Tanzania
info@mem.go.tz
www.mem.go.tz


«May 2017»
MonTueWedThuFriSatSun
24252627282930
1234567
891011121314
1516

TAARIFA KWA WAKANDARASI WALIOSHINDA ZABUNI ZA KUTEKELEZA MRADI KABAMBE WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umekamilisha taratibu za zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Turnkey III) na unawajulisha Wakandarasi walioshinda kwamba hatua inayofuata ni kupewa barua za tuzo (Award Letters) na kusaini mikataba.
Read more
1718192021
2223

UFAFANUZI KUHUSU HABARI ILIYOCHAPISHWA KATIKA GAZETI LA JAMHURI TOLEO NA. 295 LA TAREHE 23 – 29 MEI, 2017

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatoa ufafanuzi kuhusu habari iliyochapishwa katika gazeti la Jamhuri Toleo Na. 295 la tarehe 23 – 29 Mei, 2017 yenye kichwa cha habari “ Waziri apiga dili” ununuzi wa zabuni ya wakandarasi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwamba ulizingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 (kama ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2016) pamoja na kanuni zake.
Read more
2425262728
2930311234