TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTAFITI WA HALI YA UPATIKANAJI NA MATUMIZI YA NISHATI YA UMEME TANZANIA BARA KWA MWAKA 2019-2020

Wednesday, November 27, 2019|Number of views (8044)|Categories: News, Press Releases

Documents to download

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTAFITI WA HALI YA UPATIKANAJI NA MATUMIZI YA NISHATI YA UMEME TANZANIA BARA KWA MWAKA 2019-2020
Serikali inafanya Utafiti wa Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Umeme Tanzania Bara hususan katika maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics). Utafiti wa aina hii ni wa pili kufanyika ukihusisha mikoa yote ya Tanzania Bara. Utafiti wa Kwanza ulifanyika kuangalia Hali ya Upatikanaji wa Nishati ya Umeme Tanzania Bara na matokeo yalionesha kuwa upatikanaji wa umeme vijijini na mijini ulikuwa asilimia 49.3 na asilimia 67.5 sawia.

Lengo la utafiti ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Nishati ya Umeme katika ngazi ya kaya na jamii, matumizi ya umeme pamoja na faida zake kwa maendeleo.

Sambamba na ukusanyaji wa takwimu hizi, utafiti huu utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya zikijumuisha umri, jinsia, hali ya ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda na ushiriki wa jinsia zote katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Utafiti huu utahusisha jumla ya maeneo 1,250, kaya binafsi zipatazo 12,600 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatikana katika maeneo ya vijijini na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

Utafiti utafanyika kwa mfumo wa kielektroniki ambapo wadadisi watatumia kishikwambi (Tablets) kuwahoji wanakaya na viongozi wa vijiji na mitaa na kisha kujaza majibu ya mahojiano hayo kwenye madodoso. Taarifa zinazokusanywa ni siri na zitatumika kitakwimu tu kwa mujibu wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2019. Taarifa hizo zitatumika kwa madhumuni ya Utafiti huu pekee.

Aidha, taarifa zitakazopatikana zitatumika na Serikali na wadau mbalimbali katika mipango ya maendeleo.

Kutokana na umuhimu wa utafiti huu, natoa wito kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wao kutoa ushirikiano kwa wadadisi pindi watakapofika katika maeneo yao. Aidha, nitumie fursa hii kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa wadadisi kwani zoezi hili ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na marekebisho yake ya Mwaka 2019.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

E-Mail: info@rea.go.tz
Tel: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

Documents to download

«September 2021»
MonTueWedThuFriSatSun
3031123

TIME EXTENSION FOR CALL for PROPOSAL: Invitation for Financing Renewable Energy Investments in Green Mini and Micro Grids

The Rural Energy Agency (REA) announces time-extension for submission of applications for financing support from Renewable Energy Investment Facility (REIF) up to 10th September 2021, at 11:00am.
Read more
45
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930123
45678910